Je Unajua Siri ya herufi ya mwanzo ya jina lako?. Soma hapa
utaweza kuelewa Tabia zako au tabia za rafiki au mpenzi wako.
>Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa
mambo makubwa, anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu
mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda
Mamlaka, na ana kiburi, na hasira. Herufi A inawakilisha Nyota ya Punda.
>HERUFI B
>Mwenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu,
muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale
anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake. Herufi B inawakilisha Nyota ya
Ngombe,
>HERUFI C
>Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa
kukubadilika badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu na
wanaopenda mawasiliano Herufi C inawakilisha Nyota ya Mapacha,
>HERUFI D
>Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa
usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri
na wenye msimamo. Herufi C inawakilisha Nyota ya Kaa,
>HERUFI E
>Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho
nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na
mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu. Herufi E
inawakilisha Nyota ya Simba,
>
>HERUFI F
>Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye
mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu
na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi. Herufi F inawakilisha
Nyota ya Mashuke,
>HERUFI G
>Mwenye jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye
imani ya kidini na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua
matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali
ushauri wa kutoka kwa watu. Herufi G inawakilisha Nyota ya Mizani,
>HERUFI H
>Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye
ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na
bidii zake. ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi. Herufi H inawakilisha
Nyota ya Nge,
>HERUFI I
>Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu mwenye
kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira
za haraka. Herufi I inawakilisha Nyota ya Mshale,
>HERUFI J
>Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye
matamanio,mkweli, mkarimu na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio
makubwa. Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo. Herufi J
inawakilisha Nyota ya Mbuzi,
>HERUFI K
>Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri.
mwenye msimamo thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia
za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na
hali ya kimaisha. Herufi K inawakilisha Nyota ya Ndoo,
>HERUFI L
>Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa vitendo,
mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa
mara. Herufi L inawakilisha Nyota ya Samaki,
>HERUFI M
>Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye
kujiamini sana ,
mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi
kukasirika. Herufi M inawakilisha Nyota ya Punda
>HERUFI N
>Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye
ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana . Herufi N inawakilisha Nyota ya Ngombe
>
>HERUFI O
>Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra,
mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na
mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia. Herufi O inawakilisha Nyota ya Mapacha
>HERUFI P
>Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo
wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye
mambo ya watu. Herufi P inawakilisha Nyota ya Kaa
>HERUFI Q
>Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye
kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu
visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana . Herufi Q inawakilisha Nyota ya Simba
>HERUFI R
>Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye
uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda
amani. Herufi R inawakilisha Nyota ya Mashuke
>HERUFI S
>Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto
mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi
makubwa. Herufi S inawakilisha Nyota ya Mizani
>HERUFI T
>Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye
kupenda ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata
mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika. Herufi S
inawakilisha Nyota ya Nge
>HERUFI U
>Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati
kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye
tamaa na aliyekosa maamuzi. Herufi U inawakilisha Nyota ya Mshale.
>HERUFI V
>Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi,
wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika. Herufi U
inawakilisha Nyota ya Mbuzi.
>HERUFI W
>Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi,
wachangamfuu kupita kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni
watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari. Herufi W inawakilisha Nyota ya
Ndoo.
>HERUFI X
>Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa
kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na
kujitoa uaminifu. Herufi X inawakilisha Nyota ya Samaki.
>HERUFI Y (YASINTA)
>Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye
kupenda Uhuru na hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi
na husababishia kupoteza bahati katika maisha. Herufi Y inawakilisha Nyota ya
Punda
>HERUFI Z
>Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye
kupenda matumaini na amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria
kabla ya kuamua jambo. Herufi Z inawakilisha Nyota ya Ngombe.