PICHA YA ROMA NA MDOGO WAKE ALI KIBA ZAZUA UTATA MTUPU MTANDAONI

Ikiwa zimesalia wiki kadhaa ili msanii wa Hip Hop Tanzania,Roma kufunga ndoa na mpenzi wake anayejulikana kama Nancy au Mama Ivan kumeibuka na utata baada ya kusambaa kwa picha ya msanii huyo akiwa kwenye pozi linaloonekana ni la kimahaba na zabibu Kiba,mdogo wa kike wa Ali Kiba na watu kuhisi huenda wawili hao wakawa wana mahusiano ya kimapenzi.

Kituo cha redio kimoja kilimtafuta mke mtarajiwa wa Roma na kumuuliza kuhusiana na picha hiyo ambapo bibie huyo alidai kuwa hajui chochote na wala hajali kwani inaweza ikawa picha tu na shabiki na kuongeza kuwa Roma hawezi kufanya upuuzi.

Kwa upande wake Roma alipotafutwa alionekana mwenye kusita sita na kutaka kujua kama mazungumzo hayo yapo On air au Off Air,baadaye Roma alikiri kuwepo kwa picha hiyo na kudai ni ya kitambo na hakumbuki ilikuaje kwenye picha hiyo na kuomba aulizwe zaidi kuhusiana na kazi za muziki kuliko mambo mengine ya nje.