.

5/07/2016

Uchakavu Daraja la Tingetinge Wilaya ya Temeke

Baadhi wakazi wa Yombo Kilakala Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam wamelalalamikia Uchakavu wa daraja lijulikanalo kama “Daraja la Tingetinge” ambalo wamekuwa wakilitumia kwa matumizi yao ya kila Siku licha ya kwamba ni daraja la gari moshi

Daraja hilo ambalo linatajwa kujengwa Takribani miaka 40 iliyopita limeonekana kuwa Chakavu hali inayohatarisha Maisha ya wananchi wanaolitumia pamoja na Gari Moshi lenyewe jambo ambalo limeilazimu mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kuweka alama ya Tahadhari kwa watumiaji

Wakizungumza na Channel ten ambayo ilifika katika eneo hilo na Kushuhudia wakazi hao wakitumia daraja hilo licha ya kuwa na Viashiria vya kuhatarisha Maisha yao wamedai kuwa wamelazimika kutumia njia hiyo kutokana na barabara waliyotakiwa kuitumia kutokuwa Salama kwa Maisha yao.

Aidha wakazi hao wametoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua za haraka iwezekanavyo ili Kuwa nusuru wananchi na wakazi wa Maeneo hayo, huku juhudi za kuwatafuta watendaji wa eneo hilo zikiendelea kufanywa na kituo hiki