Askofu amuua muumini katika jaribio la kufanya muujiza

  Mwanamke mmoja amefariki katika misa baada ya mchungaji wa kanisa lake kujaribu kufanya muujiza.

– Mchungaji huyo wa Kanisa la Mount Zion General Assembly Afrika Kusini alikuwa akionyesha wafuasi wake uwezo wa imani

Mwanamke mmoja Afrika Kusini aliaga dunia kutokana na jaribbio la mchungaji wake kumtumia kufanya muujiza
Mchungaji huyo alikuwa akitaka kuwanyoshesha wafuasi wake uwezo wa imani kwa kutenda miujiza kama iliyokuwa ikifanywa na Yesu Kristo.

Mchungaji Lethebo Rabalungo alimuita mwanamke huyo kutoka kwa kusanyiko kanisani, na kumtaka kulala chini ambapo aliwaagiza wasaidizi kumwekelea spika kubwa mgongoni.

Wasaidizi hao walipanda juu ya spika hiyo huku mchungaji akiendelea kuelezea muujiza wake.

Kutokana na kitendo hicho, mwanamke huyo alijeruhiwa kifuani na kufariki baadaye kutokana na majeraha hayo kwa mujibu wa kituo kimoja cha radio nchini humo.

Kulingana na mchungaji huyo, mwanamke huyo alifarikia kwa sababu hakuwa na imani ya kutosha!