Breaking News: Rais Magufuli Atengua Uteuzi Wa Mkuu Wa Mkoa Arusha Felix Ntibenda,amteua Mrisho Gambo Kuwa Mkuu Wa Mkoa

Mkuu wa Mkoa mpya wa Arusha,Mrisho Gambo aliyeteuliwa na Rais,kuapishwa kesho ijumaa Ikulu jijini Dar
***

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua Bw. Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016) saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.