Makamu wa rais wa zamani wa Sudan Kusini yuko Sudan kwa matibabu

Makamu wa rais wa Sudan Kusini aliyeondolewa madarakani Riek Machar amewasili mjini Khartoum nchini Sudan kwa matibabu, limeripoti shirika la habari la serikali SUNA.

Serikali ya Sudan imesema kuwa imempokea Dr. Riek Machar, kwa sababu za kibinadamu, kutokana na kwamba anahitaji uangalizi wa dharura wa kimatibabu, kutokana na kwamba alipowasili hali yake ya kiafya ilihitaji uangalizi wa haraka wa kimatibabu.

Awali Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa alipokelewa na mojawapo ya nchini jirani kwa sababu sawa na hizo.

Hali ya kiafya ya Dr Riek Machar kwa sasa imeimarika na ataendelea kubakia nchini Sudan chini ya uangalizi kamili wa madaktari hadi atakapoondoka nchini humo kuelekea nchi nyingine atakayo ichagua kukamilisha matibabu yake.

'' Ni vema kufahamu kuwa ndugu zetu wa Sudan kusini wamefahamishwa kuhusu suala hili'' ilieleza ripoti ya serikali ya Sudan.