Mfanyakazi wa Arsenal ajiuzulu ili mshahara wake utumike kwenye usajili wa Wenger

 Mfanyakazi mmoja wa Arsenal ameamua kuacha kazi katika klabu hiyo, akimtupia maneno Arsene Wenger juu ya kushindwa kufanya manunuzi ya wachezaji katika barua yake ya kujiuzulu.

 Wenger alizidisha hasira ya mashabiki wa Arsenal aliposema kwamba kuwalipa wafanyakazi 600 ni muhimu kwake kuliko kusajili wachezaji wapya baada sare ya 0-0 dhidi ya Leicester.

Lakini mfanyakazi huyo wa Arsenal, ambaye amefanya kazi katika duka la timu, alipeleka barua ya kujiuzulu kazi kufuatia maneno ya Wenger ambaye yameleta mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii.
Katika barua yake ya kujiuzulu ameandika: “Kulaumu kwamba kuwalipa watu 600 ambao wanafanya kazi katika klabu ndio kumesababisha klabu kutosajili wachezaji ni jambo la aibu.

“Nalipwa kiasi cha £7.20 kwa saa 1, na nafanya kazi masaa 37 kwa wiki. Hivyo nalipwa £270 kwa wiki. Kwa hivyo navuna £14,040 kwa mwaka.

“Theo Walcott analipwa mara 10 ya fedha hiyo kwa wiki.

“Hivyo kwa sasa nimeamua kwamba sitoendelea kuwa mzigo kwa klabu hii.”

Sehemu ya mashabiki wa Gunners walitumia tena sauti zao kumsihi Wenger atumie fedha kusajili baada ya mchezo dhidi ya Leicester City, huku baadhi yao wakitaka kocha huyo aondoke.

Pamoja na kucheza mechi 2 tu mpaka sasa, Arsenal wamejikuta wapo pinti 5 nyuma ya vibara Manchester City, Manchester United na Chelsea.

Vilabu vya Manchester vimetumia zaidi ya  £300million katika dirisha la usajili mpaka sasa kwa dirisha hili la usajili wakati Wenger amemsajili Granit Xhaka na mlinzi Rob Holding kwa £32.5m.