Mo Farah kustaafu

Bingwa mara nne wa medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki Mo Farah anapanga kustaafu katika mbio za uwanjani baada ya kukamilika kwa mashindano ya dunia mjini London,ambapo huenda akajiunga na mbio za marathon mjini Tokyo 2020.

Farah mwenye umri wa miaka 33 ndio mwanaraidha aliyepata ufanisi mkubwa wa michezo ya Olimpiki nchini Uingereza kwa kushinda medali nyengine ya mbio za mita 5,000.

''Mwaka 2017,ningependelea kustaafu katika riadha za uwanjani na baadaye tutaona tutakachofanya katika marathon''.

Farah ambaye alimaliza wa nane alipokimbia mbio za marathon kwa mara ya kwanza mjini London miaka miwili iliopia,atakuwa na umri wa miaka 37 wakati wa michezo ya Tokyo.

''Katika mbio ndefu huwezi kujipangia kwa mda mrefu'',alisema Farah ambaye mwenzake Galen Rupp alijishindia medali ya shaba katika mbio za marathon mjini Rio siku ya Jumapili.

''Lakini huwezi kusema kwamba sitoshiriki''.