https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mwanamke aliyeolewa anaswa kitandani na wapenzi wawili | Muungwana BLOG

Mwanamke aliyeolewa anaswa kitandani na wapenzi wawili

Mwanamke mmoja ametusiwa na majirani kwa kusababisha vita.

–Jamaa mmoja aliyedai kuwa mpenzi wake alimnasa mwanamke huyo (anayedaiwa kuwa katika ndoa) na mwanamume mwingine.

Kizazaazaa kilitokea Nakuru wakati mwanamke alifumaniwa na wapenziwe wawili.

Kisa hicho kilitokea Subukia Agosti 21, ilipobainika alikuwa akishiriki uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa wanaume hao.

Kulingana na Standard, mwanamke huyo, mama wa mtoto mmoja alisikika na mmoja wa wapenzi hao aliyekuwa amemtembelea nyumbani kwake akimpigia simu mpenzi mwingine.

Cha kushangaza ni kuwa wanaume hao wameoa.

“Mmoja wa wanaume hao alikuwa akifanya ziara za mara kwa mara nyumbani humo akiwa amemnunulia bidhaa za nyumbani. Yule mwingine alidhaniwa ‘Sponsor’ kwa sababu alikuwa akizuru humo bila kubeba chochote,” Jamaa mmoja amesema.
Mmoja wa wanaume hao alisemekana kuzuru nyumba ya mwanamke huyo baada ya kujaribu kumpigia na kumkosa.

“Alipofika alipatana na mshindani wake. Alipatwa na ububu kabla ya kuketi na kuanza kumkaripia mwanamke huyo,” ilisema Standard.

Mabishano miongoni mwa watatu hao yaliongezeka na kuzua mapigano makali kati ya wanaume hao.

Mama huyo alianza kupiga mayowe, hali iliyowaamsha wanawe na majirani. Lakini badala ya kumsaidia, majirani walianza kumtusi kwa kujihusisha na wanaume wawili waliooa.