Ugaidi watajwa kuwa sababu ya Twitter kufunga akaunti za wateja 235,000

Mtandao wa Twitter umezifungia akaunti Zaidi ya 235,000 zinazojihusisha na shughuli za kigaidi katika kipindi cha miezi sita na kufikia jumla ya akaunti 360,000 kwa mwaka jana.

“kila siku tumekua tukifungia akaunti kufika mpaka zaidi ya asilimia 80% tangu mwaka jana, na zimekua zikiongezeka kila mara baada ya mashambulizi ya kigaidi” ilisema kampuni ya Twitter.

Kampuni ya Twitter ilisema kwamba inafanya kazi kwa bidii kuhakikisha akaunti ilizokua zimesimamishwa haziwezi kufunguliwa tena au kufungua akaunti zingine na kuendelea kufanya shughuli za kigaidi. Hivyo wameweza kuboresha mitambo yao na kukuza mfumo wa kiteknolojia katika mtandao wao kwani imekua ngumu kuwatambua wahusika dhahiri wa vitendo vya kigaidi katika mtandao.

“kama tulivyoeleza mwezi februari na makampuni mengine pamoja na wataalam wa mtandao kwamba haiwezekani kutambua  vitendo vya kigaidi katika mtandao”. Alisema msemaji wa kampuni, lakini kutokana na taarifa za watu juu ya tuhumu za mambo maovu tunaweza kuzitambua akaunti na kuzisimamisha.

Pia kwa kuongezea kampuni ilisema kwamba imekua ikishirikiana na makampuni mengine ya mitandao ya kijamii kupambana na watu wote wanaotumia mitandao ya kijamii kama sehemu ya kufanya shughuli za kigaidi.

“Tunaendelea kufanya kazi kwa kusimamia utekelezaji wa sheria katika idara zote huku tukiendelea na uchunguzi katika kutokomeza mambo ya kigaidi”. Alisema msemaji wa kampuni.