https://monetag.com/?ref_id=TTIb Wachina wataka kuwekeza Liverpool mzigo mnene | Muungwana BLOG

Wachina wataka kuwekeza Liverpool mzigo mnene

Mabilionea waliokuja kuwekeza kwenye vilabu vya soka nchini, Uingereza, tangu mwanzoni mwa miaka 2000, kutoka Ulaya na Amerika, wamezidi kufungua milango kwa wawekezaji wa China, nao kutaka kuwekeza kwenye ligi hiyo.

Wawekezaji wa China wanatarajiwa kununua hisa za klabu ya Liverpool zitakazokuwa na thamani ya pauni milioni 700, katika kuifanya klabu hiyo kuwa tajiri kuliko Manchester City.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali nchini Uingereza, zimesema mmiliki mkuu wa klabu hiyo John W Henry, ameshapokea maombi hayo na sasa yapo mezani yakijadiliwa.

Kampuni hiyo ya uwekezaji ya china inakisiwa kuwa na utajiri wa pauni bilioni 600.