Wanafunzi Waruhusiwa Kuingia na Bunduki Darasani

 Texas, Marekani

Mahakama Kuu ya Jimbo la Texas nchini Marekani imepitisha sheria mpya inayoruhusu wanafunzi wa vyuo ambao wamefikisha umri wa kuanzia miaka 21 kuingia na bunduki darasani ili kujilinda.

SHeria hiyo imepitishwa baada ya maprofesa wawili kushindwa kwenye ombi lao la kutaka mahakama izuiwe kutekelezwa kwa sheria mpya inayowaruhusu wanafunzi kubeba bunduki bila kuzionyesha hadharani.
Jaji katika Mji wa Austin alituzilia mbali madai ya wahadhiri hao kwamba kuwepo kwa bunduki huenda kukawa hatari kubwa iwapo mjadala mkali utazuka darasani.

Mwanasheria Mkuu wa Texas, Ken Paxton, ambaye ni wa Chama cha Republican, aliunga mkono uamuzi wa jaji, na kusema kuwa raia wanaotii sheria wana haki ya kujilinda hata wakiwa kwenye vyuo vikuu.