https://monetag.com/?ref_id=TTIb Wanaokimbia na fedha za mikopo wamkera Askofu | Muungwana BLOG

Wanaokimbia na fedha za mikopo wamkera Askofu

Singida. Waumini wa Kanisa la Pentekoste (FPCT) Tawi la Singida Mjini wametakiwa kujiepusha na tabia ya kukopa fedha kama hawana uwezo wa kuirejesha kwa wakati.

 Askofu  wa FPCT, Tawi la Singida Mjini, Dk Paulo Samwel alitoa onyo hilo jana katika ibada maalumu ya kufunga kongamano la wiki moja lililohudhuriwa na wanawake waumini wa kanisa hilo.

Alisema tabia hiyo inasababisha usumbufu ikiwamo kukimbia mji bila kupenda.

 “Tumechoshwa na malalamiko yanayohusu mikopo isiyolipika. Waumini hasa wale wanaokopa ovyo, wakati mnakopeshana mnakuwa wawili; mkopaji na mkopeshaji. Mkopaji akishindwa kurejesha mkopo mnaanza kukimbilia kwa watu. Hapana...acheni kusumbua watu malizeni wenyewe,” alisema Askofu.