https://monetag.com/?ref_id=TTIb Birdman ajipendekeza kwa Lil Wayne, ampongeza katika siku yake ya kuzaliwa | Muungwana BLOG

Birdman ajipendekeza kwa Lil Wayne, ampongeza katika siku yake ya kuzaliwa

Rapper Birdman ameweka tofauti zake (kwa muda) na Lil Wayne na kuamua kumtakia heri ya kuzaliwa msanii huyo waliyepelekana mahakamani.

Kupitia mtandao wa Instagram, Birdman amepost picha nne ambazo aliwahi kupiga na Lil Wayne na kuandika, “HBD MY SON @liltunechi#BEFORE ANYTHANG #CMR uptownshit#BMJR #ymcmb4life #bloodlove.”

Wawili hao waliingia kwenye ugomvi mzito tangu mwaka jana huku rapper huyo akitaka lebo yake ya Cash Money kumlipa kiasi cha dola milioni 51 kwa kuchelewesha kuachia albamu yake iliyotakiwa kutoka mwaka 2014