Blackberry kusitisha utengenezaji wa simu

Kampuni ya simu ya Blackberry itasitisha kutengeza simu aina ya smartphone baada ya miaka 14 katika bishara hiyo ,kampuni hiyo imetangaza.

Ikiwa wakati mmoja kiongozi katika soko la mauzo ya simu,kampuni hiyo imeshindwa katika kuhimili kasi ya mashindano na kampuni za kisasa za simu kama vile Aple na Samsung.

Mnamo mwezi Mei,afisa mkuu wa kampuni hiyo John Chen ,alisema kuwa atajua ifikiapo mwezi Septemba iwapo biashara yake ya simu itakuwa ikileta faida au la.

Blackberry sasa inasema kuwa itazitumia kampuni nyengine inazoshirikiana nazo kutengeza simu hiyo.Lakini kampuni hyo haijasema ni lini simu nyengine za Blackberry zitatolewa.

Bwana Chen amekuwa na hofu kuhusu hatma ya biashara ya simu,akisema angependelea kuifunga iwapo haitoi faida yoyote.