Dawa za kupunguza maumivu
Dawa kama vile Ibruprofen, Naproxen na Diclofenac ndizo dawa hutumiwa sana kupunguza maumivu na kuvimba.
Jarida la Uingereza la madaktari, linasema watafiti waliwachunguza watu milioni 10 , wenye umri wa miaka 77 ambao walitumia dawa hizo.
Wataalam wa Uingereza wamesema utafiti huo haukuwa na umuhimu sana kwa wagonjwa wenye umri wa chini ya miaka 65 lakini muhimu zaidi ilikuwa kwa wagonjwa wenye umri wa makamo.
Utafiti huo ulifanyiwa watu milioni 10 wanatumia dawa hizo kutoka Uingereza, Uholanzi, Italia na Ujerumani na kulinganishwa na watu wasiotumia dawa hizo.
Dawa ya kupunguza maumivu ya Ibuprofen
'Tahadhari'
Shirika la Uingereza la masuala ya moyo (BHF) limesema wagonjwa wanaougua maradhi ya shinikizo la damu, kisukari na shida za figo wanastahili kutumia dawa hizo kwa kiwago kidogo na kwa muda mfupi.
Mtu mwenye umri wa makamo
'Haswa kwa wale ambao hutumia dawa hizo za kupunguza mauamivu kila mara.'