https://monetag.com/?ref_id=TTIb Faidika na kilimo rahisi cha papai | Muungwana BLOG

Faidika na kilimo rahisi cha papai

Utafiti unaonyesha zao la mipapai ni zao ambalo halihitaji na halina gharama kubwa lakini faida yake ni kubwa sana. heka moja inachukuwa miche ya mipapai kati ya 400 au 600. mbegu zinapatikana katika kila duka la pembejeo.

Pia unaweza
kununua papai sokoni ukalila alafu mbegu ukazihifadhi kwa ajili ya kuzipanda baadae. mara nyingi mpapai hauhitaji mbolea lakini inategemea na ardhi yenyewe. mpapai unatumia miezi kati ya 9 mpaka 15 kuanza kuvuna.

Kadri mpapai unavyokaa muda mrefu ndivyo unavyodhidi kuzaa zaidi. mpapai kwa kadilio la.chini unatoa mapapai si chini ya 9 kwa kadirio la chini. pia mapapai yanaiva kwa kipindi. hivyo mapapai yanavyokomaa mara nyingi yanaiva matatu matatu mpaka manne kwa mpapai mmoja.

Sasa basi kama mpapai mmoja utakuwa unavuna mapapai manne ukizidisha mara miche uliyopanda kwa heka moja mfano miche 500. kwahiyo 4x500 utapata mapapai 2000 ukiuza kwa kila moja tshs. 500 tu. utapata tshs. 1,000,000 na hapo umevuna round moja tu. na kwa msimu unavuna mpaka round 4 kwa 7 . utakuwa na tshs. ngapi? pia zao hili halisumbui kabisa. pia mpapai unavunwa mpaka miaka 3 hadi 5 kabla haujazeeka.

Pia kwenye shamba la mipapai unaweza kupanda na mbogamboga. sasa hizo hesabu ni kwa heka 1 tu. je aliyepanda heka 2 mpaka 5 na kuendelea? mahitaji ya mapapai sokoni ni makubwa kuliko yanayozarishwa sasa. KATAA UMASIKINI SASA. wekeza kwa ajili yako na uzao wako.
MAHITAJI

Hali ya  hewa inayofaa kwa mipapai ni ya kitropik ambayo haina baridi kali na joto kiasi . Udongo usiotuamisha maji maji yakisimama kwa masaa 48 tu mpapai unaweza kufa, wenye ruruba ya kutosha kwa sababu mipapai haina mzizi mkuu haihiyaji udongo wenye kina kirefu, kipindi cha jua kali mpapai usiachwe zaidi ya wiki 8 bila kumwagiliwa maji kama hakuna mvua ingawa wakati wa mapapai kuiva kama kuna ukame basi hii huongeza ubora wa papai ikiwamo kutooza mapema sokoni

Mipapai ipandwe sehemu ambazo hazina upepo mwingi kwani huvunjika kirahisi, kama unashamba la mipapai itakubidi kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka shamba lako, miti kama miparachichi, migravilea, vibiriti (leucaena Spp) na miembe pia inafaa. Hakikisha miti ya kukinga upepo inakuwa mirefu kuzidi mipapai kwa mita 10 mpaka 20 juu zaidi Kuendelea kupanda mipapai kwenye shamba moja kunaweza kusababisha usugu wa magonjwa, nashauri baada ya miaka 3 – 5 ubadilishe zao hili angalau kwa msimu mmoja ili kuua mzunguko wa magonjwa.

Mipapai inaweza kuchanganganywa na miembe na mimea jamii ya michungwa, pia mazao ya msimu kama mahindi, mtama, ufuta , alizeti  na  mboga mboga yanaweza kulimwa. Kwa kaida kwenye mipapai kuna mipapai dume, majike  na yenye jinsia zote (multiplesex/hermaphrodite) ambayo huwa na mapapai marefu zaidi, na pia kuna isiyoeleweka ambayo huwa na mapapai mafupi sana

MBEGU
Kusanya mbegu toka kwenye mapai makubwa na yaliyo komaa na kuiva, kausha mbegu vizuri kbla ya kupanda, kama utapata mbegu za  kununua ni vizuri zaidi, baada ya kukausha hakikisha unazipanda ndani ya wiki moja Ila unashauriwa kutumiwa mbegu za hybreed chotara


KUOTESHA MBEGU
Kuna wanaopendelea kuotesha mbegu kwanza na kisha kuhamishia miche shambani, sehemu ya kuoteshea iandaliwe miezi miwili kabla, mbegu zioteshwe kwenye kina kati ya sentimeta 1 – 2 chini ya udongo wenye rutuba au pakiti za plastiki, kiwango bora cha joto ni sentigredi 21 – 27 na itachukua kati ya wiki 1 – 4 kwa mbegu kuota, kwenye kila pakiti weka mbegu 2 – 3. Panda mbegu zako kwenye kitalu kwa umbali wa sentimeta 3 toka shimo hadi shimo na sentimeta 15 kati ya mistari, hakikisha maji hayatuami kabisa, pia unaweza kupiga dawa ya copper oxychloride gramu moja katika lita moja ya maji ilikukinga miche yako na fangasi

UOTESHAJI WA MOJA KWA MOJA
Kabla ya kupanda mbegu weka mchanganyiko wa majivu na mbolea ya kuku sehemu ya kupandia, mbolea husaidia ukuaji haraka na jivu husaidia kukinga mipapai na magonjwa. Panda mbegu 3 – 5 kila shimo maana miche mingine inaweza kufa kwa magonjwa, kuliwa na wadudu au ikaota dume

KUHAMISHA MICHE TOKA KWENYE KITALU
Miche ihamishiwe shambani ikiwa na urefu wa sentimeta 20 – 40, kama udongo unatuamisha maji panda kwenye matuta yenye urefu wa sentimeta 40 – 60 mashimo yawe na ukubwa wa sentimeta 45 upana na sentimeta 30 kina na shimo lichanganywe na udongo na samadi bila kuacha kisahani cha maji, umbali ni mita 3 kwa 3 kwani mipapai inahitaji jua la kutosha.

KUPUNGUZA MIPAPAI
Baada ya miezi 3 – 5 baada ya kupanda mipapai itatoa maua na hapo jinsia ya mipapai itajulikana na mingine itabidi ipunguzwe na hasa midume, mipapai yenye jinsi zote inatakiwa isizidi asilimia 10 – 20 na midume ibaki mmoja katika kila mijike 25, mimea yenye magonjwa pia inabidi ing’olewe.

RUTUBA YA UDONGO
Weka kiasi chakilo 2 – 5 za samadi kwenye kila mpapai kwa mwaka ili kuongeza ukuaji na uzazi, mabaki ya mimea yanaweza pia kuwekwa kama matandazo na h ii ni muhimu zaidi kipindi cha kiangazi ili kuzuia unyevu usipotee.

MAGUGU
Mipapai inapopandwa tu inaweza kuwekewa matandazo kuizunguka ili kuzuia uoataji wa magugu, magugu yang’olewe yakiwa machanga na epuka kuchimbua chini sana maana mizizi ya mipapai huwa juu juu, njia nzuri ni kuweka matandazo kwenye shamba lote ili kuzuia outaji wa magugu

UANGALIZI
Mipapai iangaliwe dhidi ya magonjwa, ing’olewe na kuchomwa au kufukiwa chini ikiwa itabainika kuwa na maonjwa, piga dawa dhidi ya magonjwa ya fangasi na virusi mara yanapoibuka ili kuongeza uzaaji nakipato chako. Ondoa matawi yote yatakayojitokeza pembeni ya mpapai wako, na hii ifanyike mapema kabla ya tawi kuwa kubwa.

Ondoa mapapi yote ambayo yatakuwa hayakuchavuliwa vizuri na acha yale yenye afya tu Weka miti ya kuegemea kama mpapai utazaa matunda mengi na hasa wakati wa upepo mwingi ili kuzuia mipapai isivunjike. Mipapai ikitunzwa inaweza kuishi mika mingi, ila kwa ajili ya mazao bora ondoa mipapai na upande mingine baada ya kila miaka mitatu (3)

FAIDA
Papai zao zuri sana na kama ukipanda eka moja kwa 1000 mapapai utapata 1kila wiki, ukiuza 1000 kwa 300 tu ni laki 3 sasa ukiweka eka 5 ni 1.5m kwa wiki...dahhhh....Tanzania nzuri unataka kendwa wapi.