Kahawa yenye dawa asili ya kuongeza nguvu za kiume ndani yake yafakamiwa na wateja Marekani

 Kahawa ambayo ndani yake ina mimea asili ya kuongeza nguvu za kiume, imepata wateja wa kumwaga Marekani.

Kahawa ya Stiff Bull, imechanganywa na mimea iitwayo tongkat ali, maca na guarana (kama mkuyati wa Morogoro), inayopatikana Asia na Amerika ya Kusini ambayo wakazi wa huko wamekuwa wakiiitumia kwa kipindi kirefu.

Tofauti na Viagra, ambayo husababisha uume kupandisha mizimu baada ya kuitumia, mimea hiyo inadaiwa kuongeza homoni za mwanaume, na hivyo kumpa msisimuo asili ili kushiriki tendo hilo maarufu kwa kuongeza idadi ya watu duniani.

Sasa mimea hiyo imechanganywa kwenye kahawa inayopatikana Marekani na sasa zaidi ya wanaume 200,000 kila mwezi huiagiza mtandaoni ili iwape uhodari kitandani.

Hata hivyo mamlaka ya madawa nchini humo imeonya kuwa kahawa hiyo ina kemikali inayoweza kudhuru moyo wa mwanaume hasa ikitumiwa kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa Rais wa kampuni hiyo, Keith Hanson, kikombe kimoja kinaweza kumfanya mwanaume apate mzuka wa ajabu na kupiga mechi za kibabe!

“Ni kama kijito cha vijana cha mapenzi,” Hanson ameiambia Daily Mail Online. “It increases your stamina for sex and gives you energy, not just an erection,” anasema.