Kichaa cha mbwa, ni tisho la afya linalokuwa na kupuuzwa

Kukiwa na tishio la maradhi kama Ebola na Zika, kuna uwezekano mkubwa wa kutofikiria maradhi mengine yanayoua kama kichaa cha mbwa (rabies). Katika kuadhimisha siku ya kichaa cha mbwa duniani ambayo kila mwaka huwa sepremba 28, Umoja wa Mataifa na mashirika wadau, wanazitaka nchi zaidi kutoa kipaumbele kwa ugonjwa huo.

Kauli mbiu yam waka huu ni "Elimisha, chanja , tokomeza kichaa cha mbwa". Kila mwaka kichaa cha mbwa kinakadiriwa kukatili maisha ya takribani watu 60,000wengi wakiwa vijijini barani Asia na Afrika, na tishio linaongezeka.

Hata hivyo ugonjwa huu unaosambazwa na virusi , unazuilika kwa watu kupewa chanjo ambayo imekuwepo kwa zaidi ya karne. Hivi sasa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wanatoa wito wa kutafakari upya jinsi ya kuzilinda jamii kutopata maradhi hayo.

Kikubwa ni kutoa chanjo kwa mbwa ambao husambaza ugonjwa , lakini kama anavyoonya Silvano Sofia fkutoka shirika la chakula na kilimo FAO, ni rahisi kusema kuliko kutenda,

"Kutokomeza kichaa cha mbwa inawezekana kwa kuwapa chanjo mbwa, katika miaka ya karibuni, mtazamo umeelekweza zaidi hususani kwa magonjwa ya mifugo, kwa sababu mbwa hawana thamani ya kiuchumi na kijamii kama mbuzi na wanyama wengine wa kilimo. Hivyo tunahitaji kutoa kipaumbele katika hili".

Lengo la siku ya kichaa cha mbwa duniani ni kuelimisha kuhusu ugonjwa huo na kuchukua hatua za kuutokomeza ifikapo 2030.

Wito huo umetolewa kwa pamoja na FAO, shirika la afya duniani WHO, muungano wa kimataifa wa kudhibiti kichaa cha mbwa (GARC) na shirika la afya ya wanyama OIE.