https://monetag.com/?ref_id=TTIb Manispaa ya Temeke yagawanywa ni baada ya wilaya ya Ubungo na Kigamboni kuongezeka | Muungwana BLOG

Manispaa ya Temeke yagawanywa ni baada ya wilaya ya Ubungo na Kigamboni kuongezeka

Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo. 

Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo amesema Halmashauri ya Manispaa ya Temeke hivi sasa inagawanywa rasmi hali itakayowagawanya madiwani wa kata za eneo hilo pia.

Chaurembo akiwa katika tukio hilo  leo,  alisema mgawanyo huo umetokana na hatua ya serikali kuongeza wilaya za Ubungo na Kigamboni na kusema kuwa baadhi ya madiwani watabaki Temeke na wengine watakwenda Kigamboni.

Kwa sasa manispaa ya Kinondoni imeshagawanywa na kata 20 kati ya 34 zimebaki Kinondoni na kata 14 zipo Ubungo.