Manji Akabidhi Uwanja, Ndipo Utakapojengwa Uwanja Wa Mazoezi Wa Yanga

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameonekana “hataki mchezo” baada ya kukabidhi hati kabla ya kuanza ujenzi wa mazoezi wa kikosi cha Yanga.

Uwanja huo wa Yanga uko katika eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba alikuwepo katika hafla hiyo fupi.

Wakati Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga, Mama Karume pia alikuwa kati ya waliohudhuria shughuli hiyo.

Ujenzi utakapokamilika, Yanga itakuwa na uwanja wake wa mazoezi ambao unatarajia kuwekewa nyasi bandia.