https://monetag.com/?ref_id=TTIb Nchi 36 duniani hazina mashine za kutibu saratani | Muungwana BLOG

Nchi 36 duniani hazina mashine za kutibu saratani

Mgonjwa wa saratani 'akichomwa' kwa mashine ya kisasa na salama dhidi ya mionzi ya radiesheni aina ya cobalt 60 katika taasisi ya saratani Ocean Road

Mataifa 36 duniani hayana mashine za kutoa huduma ya kutibu saratani,hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa shirika la kimataifa la nishati ya atomiki, IAEA katika taarifa yake inayoweka bayana uwepo wa mashine hizo maeneo mbali mbali duniani.

IAEA imechapisha orodha ya upatikanaji wa mashine hizo katika vituo vya kutoa tiba za saratani ulimwenguni ambapo Marekani inaongoza kwa kuwa na mashine zaidi ya 3,200, huku baadhi ya nchi kama Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC ikionekana kuwa na mashine moja ambayo nayo nayo haifanyi kazi.
Mkuu wa kitengo cha takwimu hizo cha IAEA Joanna Izewska amesema taarifa hizo ni kutoka nchi 141 na zinaonesha maeneo ambako wagonjwa wa saratani hawawezi kupata huduma kabisa na hivyo ni fursa ya kuwezesha kupanga vyema huduma za tiba dhidi ya saratani katika nchi zinazoendelea.
Amesema ni dhahiri kuwa licha ya juhudi za miongo kadhaa za kuimarisha huduma dhidi ya saratani, bado hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa ili kuhakikisha huduma ya tiba inapatikana kwa watu wengi zaidi.