https://monetag.com/?ref_id=TTIb Ndalichako aitaka bodi ya TCU kuchapa kazi | Muungwana BLOG

Ndalichako aitaka bodi ya TCU kuchapa kazi

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameitaka Bodi mpya ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) aliyoizindua leo jijini Dar es Salaam, kushughulikia kikamilifu changamoto zilizoko katika Tume hiyo.

Profesa Ndalichako ameiambia bodi hiyo kuwa amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kuhusiana na vyuo wanavyosoma, hivyo ni wakati wa bodi hiyo kufuatilia kwa ukaribu malalamiko hayo na kuyafanyia kazi.

“Tunaelewa kwamba wanafunzi ni watu wa kulalamika kila wakati, lakini yapo malalamiko ambayo yana tija na ni lazima yatatuliwe, kwa mfano malalamiko yanayohusu uvurugaji wa matokeo au taratibu zinazokuwa kandamizi kwa wanafunzi na walimu wa vyuo vikuu,” alifafanua Profesa Ndalichako.