Utafiti wabaini Asilimia 47 ya walimu hawaingii darasani

Dar es Salaam. Utafiti mpya uliofanywa na Repoa kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa uchumi  Afrika,(AERC) umebaini kuwa asilimia 14 ya walimu hawakuhudhuria shuleni bila sababu maalumu huku asilimia 47 ya walimu hawakuingia madarasani licha ya kufika shule.

Utafiti huo uliofanywa mwaka 2014 katika sekta za afya na elimu nchini ulibaini kuwa asilimia 12 ya walimu wanatumia muda mwingi katika shughuli zao binafsi.

Katika afya utafiti huo ni asilimia 50 tu ya vituo vya afya vinavyopata umeme,maji safi na Mazingira safi.

Kadhalika ulieleza kuwa upatikanaji wa dawa muhimu katika vituo hivyo  ni asilimia 49 tu.
Uwezo wa madaktari umeonesha kuwa ni asilimia 60 ya wataalamu wanaweza kutoa tiba ikiwa ni magonjwa ya aina tatu kati ya matano ambayo walitakiwa kuyatibu.