Burkina Faso yadai kutibua jaribio la mapinduzi

Mtandao mmoja wa habari nchini Burkina Faso umechapisha maelezo ya jinsi serikali, inavyodai kutibua jaribio la mapinduzi nchini.

Koaci.com unaripoti kuwa "walinzi wa zamani wa kikosi cha ulinzi wa rais (RSP), ambao waliongoza mapinduzi yaliyotibuka mwaka 2015, walikuwa wanapanga vitendo kadhaa vya kuisambaratisha serikali," umemnukuu waziri wa usalama wa ndani Simon Compaore.

Walinzi hao 30 walikuwa wakichochea mashambulizi nchini humo, katika operesheni iliyopangwa kufanyika Oktoba 8, unamkuu waziri huyo alivyosema katika mkutano na waandishi habari.

Ameongeza kuwa na makao makuu ya jeshi katika mji mkuu Ouagadougou na kituo wanakozuliwa viongozi wa mapinduzi ya mwaka jana.

Walilenga kuetekelza mauaji pia katika kambi za jeshi na kuzusha uasi kwa kutumia mtandao wa kijamii, ameongeza Bwana Compaore.