https://monetag.com/?ref_id=TTIb Genk ya Samatta yashinda mechi ya pili Europa | Muungwana BLOG

Genk ya Samatta yashinda mechi ya pili Europa

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ametokea benchi na kuisaidia timu yake, KRC Genk kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Athletic Bilbao ya Hispania katika mchezo wa Kundi F wa Ligi ya Europa katika Uwanja wa Laminus Arena, Genk.

Katika mchezo huo ambao Samatta aliingia katika dakika ya 56 kumbadili kiungo Mbelgiji Thomas Buffel, mabao yote ya Genk yalifungwa na mabeki, Jakub Brabec kutoka Jamhuri ya Czechoslovakia katika dakika ya 40 na Mnigeria Onyinye Wilfred Ndidi katika dakika ya 83.

Kwa matokeo hayo, Genk sasa inaongoza Kundi F kwa kufikisha pointi sita baada ya mechi tatu, ikishinda mbili na kufungwa moja.