Guardiola: Iwapo Sergio ataamua kuondoka utakuwa ni uamuzi wake

Kocha wa timu ya Manchester City Pep Guardiola amesema Sergio Aguero na Vincent Kompany hawa wote wana miaka ya ziada katika klabu hiyo ya ligi ya Uingereza.

Wachezaji hao hawakucheza katika mchuano wa ligi ya ubingwa wa Ulaya dhidi ya Barcelona ambapo Man City ilifungwa.

Kompany hakuwepo hata kwenye benchi, jambo lililozusha tuhuma kwamba huenda wanasoka hao hawapo katika mipango ya Guardiola.

Baadae kocha huyo raia wa Uhispania amesema: “Vincent alikuwa hayuko sawa kucheza. Sergio, nilisema baada ya mechi, ilikuwa ni uamuzi wa kiufundi.

“Iwapo Sergio ataamua kuondoka, utakuwa ni uamuzi wake.”

Uamuzi huo wa kutomchezesha Aguero na Kompany umezusha maswali, kama ilivyo kwa utendaji wa kipa Claudio Bravo, aliyeondolewa Nou Camp, na mbinu yake ya kumiliki mpira, ambayo Guardiola amesema mara kwa mara hatoibadili imezusha shutuma.

“Mustakabali wa Vincent na Sergio upo Manchester City. Atakapokuwa sawa, ni mchezaji mzito wa kiungo cha ulinzi. Nampenda. Katika suala la Aguero, ulikuwani uamuzi wa kifundi. Nilitaka mchezaji mmoja wa ziada wa kiungo cha kati . Najaribu kuudhibiti mpira, kwasababu ukiwa nao, Lionel Messi, Neymar na hata Luis Suarez hawaupati.