Jifunze Kuendesha Kilimo Hiki Cha Kisasa, Ili Uweze Kutoka Kwenye Umaskini

Katika makala yetu ya leo  tutaangalia namna unavyoweza kuendesha kilimo bora cha kisasa ili uweze kukabiliana na changamoto za maisha ikiwemo na kuutokomeza umaskini kabisa.

Ikumbukwe kwanza kuna aina mbili kubwa za kilimo. Aina ya  kwanza ni kilimo cha nje yaani ‘outdoor farming’. Hiki ni kilimo ambacho hutegemea mvua au  umwagiliaji, lakini mkulima hana uwezo wa kutawala kiasi cha maji au kiasi cha jua. Mazao huweza kuzalishwa nje kama ambavyo wakulima wengi tumezoea kuwaona.

Aina ya pili ni kilimo cha greenhouse/ kitalu nyumba
Kilimo hichi hufanyika ndani ya nyumba maalumu iliyotengenezwa kwa kutumia aina maalumu zinazoruhusu mwangaza kupenya ndani.

Pembeni huzungushiwa wavu maalumu unaoruhusu hewa kuingia na kutoka. Na chini huwekewa mipira maalumu kwa ajili ya kufanya umwagiliaji wa zao lako.

Faida za kulima kwenye kitalu nyumba/greenhouse.  Mkulima anaouwezo wa kudhibiti hali ya hawa mfano kiwango cha maji yanayohitajika, kiwango cha joto, kiwango cha unyevu angani/ humidity. Na hivyo kumruhusu mkulima kufanya uzalishaji hata wakati ambapo mvua kubwa zinaendelea kunyesha sehemu mbali mbali.

‘Greenhouse’ inapunguza mashambulizi ya wadudu waharibifu kwakua nyumba huzungushiwa wavu maalumu hupata mavuno mengi zaidi kwenye eneo dogo kutokana na mazingira maalumu ya uzalishaji. Mfano kwenye greenhouse’ yenye ukubwa wa mita 8 kwa mita 15 ambapo huingia miche 500 ya nyanya mkulima huweza kuvuna kuanzia kilo 5000 (tani 5) za nyanya na kuendelea.

Cha muhimu kukumbuka, kuwa na greenhouse pekee sio uhakika wa asilimia zote kukupatia mazao mengi kwasababu ni lazima iendane na upandaji wa mbegu bora ambazo ni maalumu kwa kilimo cha greenhouse.
Lazima uandae shamba lako vema kwa kulima vizuri na kuweka mbolea samadi yakutosha. Lazima umwagilie kwa wakati. Lazima pia uzingatie udhibiti wa wadudu na magonjwa.

Wakulima wengi wanaolima kizamani wanalalamika kilimo hakilipi na kweli kilimo cha kizamani hakiwezi kukulipa kamwe yaani Kilimo cha zama za kwanza za mawe. Kwa mfano watu wanaolima kwa kuangalia angani walioapanda matikiti kwa kutumia mvua za mwezi wa 11 sasa hivi wamevuna na wamejaza matikiti sokoni hayana wateja.

Hiyo ni kwa sababu kila mtu anaweza kulima tikiti kirahisi wakati mvua ya vuli iliponyesha. Sio wote mnakutana sokoni muda huu. Vile vile wakulima wakizamani muda wa miezi ya kwanza au ya pili hawawezi kulima sana nyanya kwa kuwa mabonde yao yamejaa maji na pia wanaogopa kupambana na magonjwa ya aina mbalimbali.

Matokeo yake wanajikuta wakipishana na pesa ambapo mwezi wa pili au watatu nyanya bei yake inakuwa juu sana. Sasa basi kumbe muda huu ungekuwa na kitalu nyumba/greenhouse ndio ilikuwa muda wako wakuvuna pesa mpaka mwezi wa sita wakati wale wanaosubiri kilimo cha kuangalia juu watakapoenda shamba.

Kwa kawaida green house zipo za aina tofauti kulingana na mkulima  anavyotaka iwe. Huwa zipo ‘greenhouse’ za ukumbwa kama huu;

Greenhouse ya ukubwa wa mita 8x15 ni shilingi milioni 4.5

Greenhouse ya ukubwa wa mita 8 x20 ni shilingi milioni 5.5

Greenhouse ya ukubwa wa mita 8x30 ni shilingi milioni 7.5

Greenhouse ya ukubwa wa mita 8x40 ni shilingi milioni milioni 8.5.

Kwa mkulima yoyote anayehitaji huduma ya kutengenezewa Greenhouse atafuatwa popote pale alipo na kampuni yetu bila bei yoyote kubadilika. Mkulima atapewa somo la zao analotaka kuzalisha na utunzaji wake mpaka atakapovuna.

Kama unataka kufahamu vizuri zaidi juu ya kilimo hiki au unahitaji huduma ya kufungiwa Greenhouse, popote ulipo wasiliana naye kwa email jmabagala@gmail.com au 0754 282 448