Mjadala wa muswada wa sheria ya huduma za habari waendeleo mjini dodoma chini ya kamati ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii

 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ikiendelea na majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba (kulia) akielezea jambo kwa wajumbe wa Kamati yake na viongozi na watendaji wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakati wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye .

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kushoto) akijibu hoja mbalimbali za wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba .

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akisisitiza jambo kwa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson (kushoto) akifafanua jambo wakati wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma.


 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akijibu hoja zilizotolewa na baadhi ya wajumbe ambao wanashiriki kuuchambua Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia majadiliano na hoja mbalimbali katika kikao cha kuujadili Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari kinachoendelea Mjini Dodoma leo Oktoba 21,2016.Picha zote na Idara ya Habari MAELEZO