https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mourinho: Pogba anahitaji apewe muda zaidi Man Utd | Muungwana BLOG

Mourinho: Pogba anahitaji apewe muda zaidi Man Utd

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema kwamba hakutarajia mchezaji Paul Pogba, ambaye alicheza vyema sana dhidi ya Fenerbahce katika ligi ndogo ya Ulaya, azoee soka ya England haraka.

Amesema mchezaji huyo anatakiwa kupewa muda kuzoea kucheza tena England badala ya kukosolewa kila mara.

Pogba, 23, ambaye ni mchezaji ghali zaidi dunian aliyenunuliwa £89m mwezi Agosti na kuvunja rekodi ya dunia, alifunga mabao mawili Alhamisi wakati wa ushindi wao wa 4-1 dhidi ya Fernabahce.

Hata hivyo hakung’aa Jumatatu dhidi ya Liverpool mechi waliyotoka sare 0-0.

“Siku mbili zilizopita, alitajwa kuwa mchezaji mbaya zaidi katika Ligi ya Premia na saa 48 anasifiwa sana,” amesema Mourinho.
“Anahitaji muda. Naridhishwa na uchezaji wake. Ana ustadi tunaohitaji.”

Mourinho ameongeza kusema anaamini Pogba bado anazoa aina tofauti ya soka.

“Nilikuwa Italia na nafahamu sifa za soka huko, kasi yake na ukali wake,” Mourinho, 53, alisema.
“Kuwa Italia kwa miaka minne au mitano na kisha urejee Ligi ya Premia, sikumtarajia aanze mara moja kung’aa.”