Mwenyekiti wa Uvccm leo amefanya ziara ya kuyatembelea mashina Arusha

Mwenyekiti wa Uvccm leo amefanya ziara ya kuyatembelea mashina ya wakereketwa kwenye kata za unga Ltd Ngarenaro na Levolosi

kwenye ziara yake alilenga kusikiliza kero za vijana pamoja na kuimarisha jumuia

katika shina la Mikokoteni lililopo kwenye soko la kilombero vijana wameelezea kuridhishwa na kasi ya utendaji ya serikal ya awamu ya tano pia wameonyesha kuridhishwa kasi ya wayeule wa rais ndani ya mkoa na wilaya yetu wamemzungumzia Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwa utendaji wake wakazi ambao unalenga kuwasaidia wananchi vile wamefurahishwa Kwa kitendo cha halmashaur kuzuia  posho ambazo madiwani walijiongezea kinyume cha utaratibu wamemtaka mkurugenzi wa jiji Ndugu Athumani Kihamia  kutolegeza kamba kwenye jambo hili la posho japo limemjengea uadui mkubwa sana Kwa madiwani

katibu wa shina  la serikali mbili ameelezea masikitiko yao Kwa mwkt wa Uvccm wilaya juu ya kitendo cha aibu kilichofanywa na mbunge wa Arusha kwenye uzinduzi wa Hospital ya HUDUMA YA MAMA NA MTOTO Kwa kuingilia hotuba ya Mhe mkuu wa mkoa wakati akihutubia jambo lile limetudhalilisha sana kama wanaarusha mbele ya wageni wetu wale tumshukuru sana mkuu wa mkoa kwa busara zake alizotumia maana angetumia nguvu ya dola kumdhibiti Lema ingejenga sifa mbaya sana kwetu kama watu wa Arusha ila sisi kama vijana tunawaomba hao wafadhili waendelee sisi wananchi na serikal yetu tupo nao

baada ya ziara hiyo namwkt kumaliza kuzipokea kero za vijana wake amewahakikishia kurudi tena na kero zao amezichukua atakaa na Mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa jiji kwaajili ya kuzipatia ufumbuzi