Paul Makonda ametangaza kuwazadia million 2 kwa wanafunzi wa kidato cha Nne watakaofanya vizuri masomo ya sayansi

Mkuu wa Mkoa wa dsm Paul Makonda ametangaza kuwazadia shilingi million mbili kwa wanafunzi wa kidato cha Nne watakaofanya vizuri katika masomo ya sayansi,ambapo wa kwanza,wa pili na watatu lakini pia watasoma bure miaka miwili ya kidato cha 5 na 6 huku watakaofanya vizuri kidato cha sita watasomeshwa bure katika chuo chochote jijini dsm.

Aidha Makonda ametoa zawadi ya shilingi million 2 pia kwa kila mwalimu wa sayansi atakayewezesha mwanafunzi kufaulu somo lake na kupewa safari ya siku mbili kutembelea mbuga za wanyama ili apumzike na familia yake.

Makonda ametoa wito huo wakati wa mahafari ya kidato cha nne ya shule ya sekondari ya St.Joseph inayomilikiwa na kanisa katoliki jijini Dsm.

Aidha Mkuu wa mkoa amewataka walimu jijini dsm kufanya kazi kwa bidhii na kujituma wakati serikali ikiendelea kujipanga kwa kuboresha maslahi yao lakini pia kuziba mianya iliyokuwa ikitumiwa na watumishi wasikuwa waadilifu,kwa kupandikiza wanafunzi hewa,walimu hewa ambapo walikuwa wachangia kuongeza gharama zisikuwa na tija.