Paul makonda amewataka wakazi wa jiji la Dsm hususan wafanyabiashara kutumia fursa ya Ujio wa Mfalme wa morroco wa 4

Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda amewataka wakazi wa jiji la dsm hususan wafanyabiashara kutumia fursa ya Ujio wa Mfalme wa morroco wa 4 anayetarajia kuingia nchini siku ya jumapili kujenga mahusiano ya kibiashara pamoja sekta ya utalii.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dsm Bw,makonda amesema Mfalme huyo wa morroco atafuatana na Msafara wa wafanyabiashara zaidi ya Elfu moja ambao pamoja na mambo mengine watakutana na wafanyabiashara wa Tanzania katika kuangalia maeneo ya uwekezaji,utalii lakini pia usafirishaji bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

Miongoni mwa mikataba itakayosainiwa kati ya Tanzania na Morroco ni pamoja na Ujenzi wa reli kutoka kilwa hadi mtwara,mikataba ya kusaidia sekta ya kilimo pamoja biashara.

Aidha Mkuu wa mkoa amewataka wakazi wa jiji la dsm kujitokeza kwa wingi wakati wa ujio wa Mfalme huyo lakini pia amewataka wananchi kuwa wavumilivu hasa pale barabara za nyerere,gerezani,sokoine na stesheni wakati Msafara wa Mfalme huyo atakapopita.