Serikali lawamani

Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Ruth Mollel ameikosoa Serikali akidai imekithiri kwa ukiukwaji wa sheria za utumishi.

Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari jana, Mollel ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chadema, amesema ameshuhudia ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Utumishi wa Umma ya Mwaka 2002 kuhusu suala la nidhamu kwa watumishi tangu Serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli iingie madarakani.

“Tumeshuhudia baadhi ya viongozi wa kisiasa kama mawaziri, naibu mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya wakiwawajibisha watumishi ilhali hawana mamlaka hayo kisheria,” amesema.