Songwe kupata wataalamu wa mazingira

Waziri wa Nchi, Ofisi  Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesema atazungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais(Tamisemi), George Simbachawene kwa ajili ya kuajiri wataalamu wa mazingira wa mkoa huo.

Makamba amesema Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 inampa mamlaka waziri wa Tamisemi kuajiri au kuteua  mtaalamu wa mazingira wa mkoa husika ambaye atakuwa kiungo kati ya mkurugenzi wa mazingira na baraza lake.

Waziri huyo amefikia uamuzi huo baada ya kupewa taarifa  uongozi wa Songwe kuwa  mkoa huo mpya hakuna mtaalamu wa mazingira, hali inayosababisha kushindwa kufanya shughuli zake kwa ufanisi.

Ofisa Mazingira wa Halmashauri ya Mbozi, Hamis Nzunda amesema endapo  mtaalamu huyo akiajiriwa atakuwa msaada mkubwa mkoani humo.