https://monetag.com/?ref_id=TTIb Takwimu: watanzania wengi bado Maskini | Muungwana BLOG

Takwimu: watanzania wengi bado Maskini

Serikali imesema licha ya kushuhudia takwimu za ukuaji wa uchumi wa taifa katika muongo mmoja iliyopita, karibu theluthi moja ya wananchi wa Tanzania bado ni masikini  wanaishi katika mazingira hatarishi.tasaf

Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Peter Ilomo amebainisha hayo kwenye uzinduzi wa matokeo ya awali ya tathmini ya mpango wa kunusuru kaya masikini Tanzania TASAF unaotekelezwa awamu ya tatu, ambapo amesema wakati ukuaji wa uchumi wa taifa unakua kwa wastani wa asilimia 7 kwa mwaka, Lakini kiwango cha umasikini kimekuwa kikipungua kwa kasi ndogo mno..

Nao wadau walioshiriki katika utafiti huo wametoa mapendekezo kadhaa ikiwemo kuwepo haja ya kuwa na dhamira ya muda mrefu katika mpango ili kuendeleza kizazi cha vijana chenye afya na elimu bora.