TFF yataka Simba na Yanga wamalizane kuhusu Kessy

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF, limeendelea kutoa ufafanuzi juu ya suala la mchezaji Hassan Ramadhani Kessy kuhusiana na madai ya klabu ya Simba ya mchezaji huyo kuvunja mkataba.

Afisa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba mchezaji huyo yuko huru kucheza mechi za ligi kuu ya Tanzania bara kwa kuwa kamati ya hadhi ya wachezaji ilimuidhinisha kuichezea klabu ya Yanga kwasababu viongozi wa Simba hawakuwasilisha kesi inayohusiana na masuala ya usajili.

Lucas amesema kwamba klabu ya Simba imewasilisha kesi ya madai hivyo ni jukumu la pande hizo ziweze kukubaliana jinsi namna gani wanavyoweza kulimaliza suala hilo.