Vurugu za wenyeviti wa mitaa Mwanza zasababisha mkutano Kuvunjika.

Vurugu kubwa zimeibuka na kusababisha mkutano wa mkuu wa wilaya ya Nyamagana kuvunjika, baada ya wenyeviti 174 wa serikali za mitaa katika halmashauri ya jiji la Mwanza kutoka nje wakipinga agizo la mkurugenzi mtendaji wa jiji hilo la kuwanyang’anya mihuri, ili wakabidhiwe maafisa watendaji wa mitaa.

Mkutano huo uliokuwa chini ya uenyekiti wa mkuu wa wilaya ya Nyamagana ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo Mary Tesha Onesmo umeingia doa baada ya wenyeviti hao kuamua kutoka ukumbini, je nini msimamo wao kufuatia agizo hilo ?.

Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Manza kiomoni Kibamba, akazungumza na waandishi wa habari kuelezea sababu za wenyeviti hao kunyang’anywa Mihuri.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mary Tesha Onesmo akifungua mkutano huo aliouitisha ili kukumbushana majukumu yao ya  aliwataka wenyeviti wa serikali za mitaa, watendaji wa mitaa na watendaji wa kata kuwatumikia wananchi katika shughuli za maendeleo na kutokuwa chanzo cha migogoro.