Waziri Makamba kuitangaza Mbeya Mountain Range kuwa eneo la Mazingira Nyeti

Ikiwa ni siku ya tano kati ya 16 za ziara yake katika mikoa 10, Mhe. January Makamba, Waziri wa Mazingira na Muungano ofisi ya Makamu wa Rais akiwa mkoani Mbeya  ametangaza eneo la Mbeya Mountain Range kuwa ni eneo la ‘MAZINGIRA NYETI/ENVIRONMENTALLY SENSITIVE AREA". ambapo Wiki ijayo uamuzi huo utapelekwa kutangazwa kwenye ‘Government Gazette” kupelekea usimamizi wake kuanza rasmi.

Kwa kuzingatia kifungu cha Sheria ya Usimamizi ya Mazingira ya Mwaka 2004, Agizo hilo la Makamba amelitoa kwa  kutumia kifungu nambari 51 Kinachomtaka Waziri husika atakapoona inabidi, anaweza kutangaza kwa amri itakayotangazwa kwenye Gazetli la Serikali, eneo lolote kuwa mazingira nyeti kwa mujibu wa Sheria hii. ambapo hii ni mara ya kwanza kifungu hiki cha Sheria hii kinatumika. Waziri Makamba aliongeza na kusema “Hapa ndio eneo la kwanza, lakini tuna nia ya kutangaza mengine mengi zaidi”.

Hatua hiyo imefuata baada ya Eneo la Mbeya Range Mountains kuwa likiathirika kwa ukataji miti hovyo pamoja na ukataji unaofanywa ki biashara kwa ajili ya mahitaji mbali mbali ya miti ikiwa ni pamoja na nguzo za umeme unaofanywa na Tanzania Forestry Services (TFS) pamoja na wafanyabiashara wa mkaa.

Hata hivyo Mheshimiwa January Makamba alisema pia amealizaimika kufanya hivyo kwasababu vyanzo vya maji yanayokuja Mbeya yanatokea huko lakini watu wameshindwa kabisa kudhibiti uharibifu wa vyanzo hivyo na kueleza kuwa miaka ya nyuma kulikuwa na vyanzo 49 lakini sasa vimebakia 4. 


Licha ya kuelekeza milima hiyo kuanza kupandwa kwa miti ya asili inayohifadhi maji, Mbeya Mjini kwasasa inahitaji lita milioni 50 za maji kwa siku, kutokana na uharibifu wa vyanzo vya maji katika safu za Milima ya Mbeya, ifikapo mwaka 2018, maji katika mji wa Mbeya hayatawatosha wakazi wa Mbeya.


Waziri January Makamba alianza ziara yake tarehe 16/Oktoba/2016 ya kutembelea  mikoa 10 ya Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora na Dodoma. Mikoa hii imeathirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi na kuporomoka kwa hifadhi za mazingira kwa ujumla nchini.