Kiwanda cha Saruji cha Dangote Kimesitisha Uzalishaji

Kiwanda cha Saruji cha Dangote kimesitisha uzalishaji kutokana kuelemewa na gharama za uendeshaji hatua inayowaacha watumiaji wake njia panda.


Mwezi uliopita Kiwanda hicho kilililamikia Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini(TPDC) kwa kushindwa kuwauzia gesi kwa bei rahisi wakati inazalishwa mkoani Mtwara.

Picha inayohusiana

Pia kiwanda hicho kinapinga uamuzi wa serikali kupiga marufuku kiwanda chake kuingiza makaa ya mawe kutoka Afrika Kusini na kutakiwa kutumia ya Liganga ambayo yapo chini ya kiwango na bei ghali.