Serikali yasema haikusudii kutumia umeme wa mafuta laba ikitokea itatumia kwa dharura.

Serikali imesema haina dhamira ya kuendelea kutumia umeme wa mafuta kama utakuwepo ni kwa dharura, kwa kuwa  una gharama  kubwa na ndiyo maana inafanya jitihada za kuiunganisha mikoa ya Ruvuma na Njombe na umeme wa gridi ya taifa ambao utakuwa suluhisho la kukatika kwa umeme katika  mikoa hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dakta. MEDARD KALEMANI kwa nyakati tofauti katika Wilaya za  Songea na Nyasa.

Amesema mradi wa Makambako-Songea utakuwa suluhisho la matatzo ya umeme kwa mikoa  ya Ruvuma na Njombe.

Awali akiwa Wilayani Songea ,   Mkuu wa wilaya  hiyo, POLOLETI KAMANDO MGEMA  amemueleza  Naibu Waziri  kuhusiana na matatizo ya umeme katika wilaya hiyo yanayotokana  na uchakavu wa mitambo iliyozinduliwa mwaka  1967 ambapo ameuagiza uongozi wa  Shirika la Umeme  Tanzania - TANESCO Mkoani Ruvuma kushughulikia  tatizo hilo.