Wapangaji jengo la Quality Plaza wametekeleza Amri ya Mahakama kuu kitengo cha ardhi cha Kuondoka katika jengo hilo


Wapangaji katika jengo la Quality Plaza lililopo barabara ya Nyerere jijini Dsm wametekeleza Amri ya Mahakama kuu kitengo cha ardhi cha Kuondoka katika jengo hilo baada ya kutolewa saa 24 ambazo zimemalizika asubuhi ya leo,huku kampuni ya Yono ikisimamia zoezi hilo lililoendeshwa Chini ya Ulinzi mkali .

Majira ya Saa mbili Asubuhi Channel ten imeshuhudia wapangaji katika jengo hilo wakihamisha samani zao,huku ikielezwa kuwa makampuni zaidi ya matano yaliyopangishwa chini ya Kampuni mama ya Quality Group ilianza kuondoa mali zao usiku wa kuamkia leo.

Scolastica Kevela – Mkurugenzi
a Yono.
Mkurugenzi wa Yono ambayo imepewa Kibali cha kuwahamisha wapangaji hao na Mfuko wa hifadhi ya jamii -PSPF amesema jengo hilo hivi sasa liko chini ya Usimamizi wao mpaka pale wapangaji wote watakapondoka. w

Dalali wa Mahakama kuu kitengo cha Ardhi Yono Steven Kevela amesema zoezi hilo la kuwahamisha wapangaji sugu wasiolipa pango na kukamata mali zao na kuzipiga mnada litaendelea kwa kasi na kuwataka wote waliopewa notisi za kulipa katika kipindi cha Siku saba kutekeleza kinyume chake sheria itachukua Mkondo wake.