Akamatwa kwa kutuhumiwa kuuza bima feki mkoani Morogoro.

Mwanamke mmoja mkazi wa Bomarodi manispaa ya Morogoro Neema Monyo amekamatwa na maafisa wa mamlaka wa usimamizi wa bima  kanda ya kati (TIRA) kwa kushirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kwa madai ya tuhuma za kukutwa akiuza bima feki kinyume na taratibu kunakopelekea kuikosesha serikali mapato.

Bi.Neema amejikuta akiwa katika wakati mgumu  mara baada ya mama mmoja aliyeuziwa bima ambayo ilionekana kuwa ni feki kukamatwa katika operesheni ya kukagua bima feki inayoendelea mkoani hapa kisha kumtaja aliyemuuzia na kukamatwa na kuwekwa nguvuni.

Naye mama aliyedai kuuziwa bima hiyo feki Flora Musiba amesema yeye wakati ananunua hakujua kuwa nifeki na baada ya gari yake kukamatwa akawasaidia maafisa hao kuwaonyesha aliyemuuzia.

Kwa upande wake meneja wamamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania (TIRA) kanda ya kati Stela Rutaguza amesema wamemkamata muuzaji huyo kisha wanamfikisha  katika  kituo cha polisi kumfungulia mashita kwa uuzaji wa bima feki.