VIDEO:Rais Magufuli akitangaza kupandisha mishahara



Rais John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa kuanzia mwezi Novemba mwaka huu serikali ya awamu ya tano itawapandisha vyeo na kurekebisha mishahara ya watumishi 59,967 baada ya zoezi la uhakiki wa vyeti feki na hewa kukamilika

Rais Magufuli amesema hayo leo kwenye sherehe za maazimisho ya mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu za miaka 18 ya kifo cha Baba wa Taifa  Mwalimu Nyerere sherehe ambazo zimefanyika visiwani Zanzibar.  Rais Magufuli katika hotuba hiyo alitolea mfano uzalendo wa Baba wa Taifa ambaye aliamua kupunguza mshahara wake na kukata kuongeza mishahara ya watumishi wachache huku walio wengi wakipata shida.

“Ninaposema hivyo simaanishi kuwa mishahara isiongezwe. La hasha. Ninachosema ni kwamba kabla ya kudai nyongeza ya mishahara ni lazima kwanza kufahamu uwezo wa Serikali, lakini pia tutambue kuwa kuna Watanzania wenzetu wengi tu wanaohitaji kuboreshewa huduma" Alisema
Rais Magufuli 

TAZAMA FULL VIDEO HAPO CHINI