Kuwait yaungana na Tanzania

Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem ameungana na mamia ya viongozi wa Serikali akiwemo Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali katika uwanja wa ndege wa Zanzibar, ameungana nao kupokea na kuaga miili ya wanajeshi wa Tanzania waliopoteza maisha yao huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakilinda amani chini ya muavuli wa umoja wa mataifa.

Al- Najem amesema kuwa Serikali ya Kuwait inalaani vikali tukio la kushambuliwa wanajeshi wa Tanzania na kupelekea wanajeshi 14 kufariki huku wengine 44 wakijeruhiwa. Ameongeza kuwa' tumefuatulia tukio hili la kushambuliwa wanajeshi wa kulinda amani katika kambi yao huko Kongo kwa huzuni kubwa, ambapo Serikali ya Kuwait inakemea
vikali mashambulizi yanayolenga vikosi vya kulinda amani au mashirika ya kibinadamu'.

Hayo ameyasema wakati wa ziara yake ya kikazi visiwani Zanzibar, Balozi Al-Najem amuomba Mwenyezi Mungu awarehemu wanajeshi waliouwa na kuwaponesha kwa haraka waliojeruhiwa

Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi aongoza mamia kupokea na kuaga miili ya wanajeshi wa Tanzania waliopoteza maisha yao huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakilinda amani chini ya muavuli wa umoja wa mataifa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar,