Loading...

3/24/2018

Kipa wa Singida United arejea kuikabili Yanga

Kuelekea mchezo wa robo fainali Kombe la Shirikisho nchini (ASFC) kati ya wenyeji Singida United dhidi ya Yanga SC, mlinda mlango Manyika Jr amerejea baada ya kuwa nje kwa muda mrefu.

Manyika Jr alipata majeraha ya goti ambayo yamemweka nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja lakini sasa amemaliza matibabu yake ambayo alikuwa anafanyiwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na yupo tayari kuanza kucheza.

''Mchezaji wetu Peter Manyika Jr aliyekuwa nje ya uwanja akikabiliwa na majeraha kwenye goti, ameshamaliza matibabu yake na tayari atajiunga na wenzake kuanza mazoezi'', imeeleza taarifa ya klabu hiyo.

Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Namfua mjini SIngida ambapo mshindi atatinga hatua ya nusu fainali wa kombe hilo. Bingwa wa michuano hiyo anapata nafasi ya kuwakilisha taifa kwenye kombe la Shirikisho Afrika.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger