4/19/2018

Diamond: Mpeni salamu zangu King Kiba

Ikiwa leo April 19, 2018 msanii Alikiba ameoa, mshindani wake kimuziki Diamond Platnumz hajakaa kimya kwenye hilo.

Diamond amefunguka kuwa amepewa taarifa za Alikiba kuoa siku ya leo, hivyo amemtumia salamu na kumtakia maisha mema ya ndoa. Kupitia ukurasa wake wa Intagram tumegulia kile alichogusia kuhusiana na ndoa ya Alikiba;

“Wadau Nimeambiwa King Kiba kaoa leo, mpeni Salam zangu za ndoa njema na Maisha yanye Furaha, Amani na Baraka tele,” amesema Diamond.

Msanii Alikiba amefunga ndoa na mpenzi wake  Aminah Rekish asubuhi ya leo mjini Mombasa nchini Kenya. Pia Utakumbuka Diamond alishaweka wazi mipango yake ya kuoa mwaka huu.