Kesi ya Aveva, Kaburu yahirishwa

Mahakam ya  Hakimu Mkazi Kisitu imeahirisha kuwasomea maelezo ya awali rais  wa klabu ya Simba Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’, kwa sababu Hakimu anayesikiliza kesi hiyo hayupo

Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leonard Swai mbele ya Hakimu Mkazi Matha Mpanze alidai kuwa kesi hiyo imekukuja kwaajili ya kusomewa maelezo ya awali lakini Hakimu Thomas Simba hayupo.

Baada ya kutolewa kwa Maelezo hayo, Hakimu Mpanze aliahirisha kesi hiyo hadi April 30,2018 kwaajili ya kusomewa maelezo ya awali.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi na kutakatisha fedha dola za kimarekani 300,000.

Miongoni mwa mashtaka hayo, Katika shtaka la kwanza, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa  walikula njama ya kughushi fomu ya maombi ya kuhamisha fedha ya March 15,2016 wakionesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa  dola za kimarekani 300,000 kwa Evans Aveva wakati si kweli.

Inadaiwa kuwa March 15,2016 katika benki ya CRDB tawi la Azikiwe Ilala Aveva akijua alitoa nyaraka za uongo ambayo ni fomu ya maombi ya kuhamisha fedha.