5/16/2018

Kama Unasumbuliwa na Kichomi

VIJANA wengi leo nyumbani Bongo wanapatwa na maradhi ambayo zamani yalikuwa ya wazee au watu wa makamo. Maradhi haya ni kama kisukari na mstuko wa moyo.

Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya. Ukipatwa muda mrefu au kila wakti ; basi …chunguza zaidi.

Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa.

  1. Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidi
  2. Dalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic
  3. Dalili za minyoo

Jambo la kuangalia ni je?

  1. Unashikwa kichomi ukiwa unatembea?
  2. Umeinama au umelala
  3. Ukishakula chakula

Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina maana kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo.

Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina maana kuna tatizo katika chakula unachokula. Je mlo wako una acid(uchachu) sana? Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa wingi sana? Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimeng’enyui sawasawa linachoka.

Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku. Mathalan usiweke pilipili katika kila mlo.

Tatizo jingine ni ulaji wa chakula chenye chumvi nyingi sana. Chumvi inakorofisha pia mzunguko wa damu mwilini.hasa kama hunywi maji.