Nape asema hawezi kukubali

Mbunge wa Mtama (CCM) Nape Nnauye amesema kwamba hawezi kukubali bajeti ya kilimo ipite kwasababu wananchi wake pamoja na wakulima watamshangaa kwa kukubali bajeti hiyo ambayo haina uhalisia kwa maisha ya mtanzani hasa mkulima.

Nape amesema hayo Bungeni leo Mei 16 wakati wa kuchangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi katika wizara ya kilimo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na kumtaka waziri husika asione tabu kwenda kuingalia upya bajeti hiyo.

“Bidhaaa ambazo wananchi wanatakiwa kuuza bidhaa zao na wakanunue bidhaa kama sukari, mafuta ya kula na vitu vingine vyote vimepanda sana, sasa uhalisia unakataa, mimi nikikubali wananchi wangu, wakulima wa mbaazi, ufuta, pamba na wakulima wengine wote nchi hii watanishangaa” amesema Nape

Mbunge huyo ameongeza kwamba katika mwaka wa fedha 2016/2017 serikali ilitenga 0.93% ya bajeti katika wizara ya kilimo na katika mwka wa fedha 2017/2018 bajeti ikapungua mpaka kufikia 0.85% na mwaka mpya wa fedha 2018/2019 imezidi kushuka mpaka 0.52%

Nape alisema serikali ya awamu ya tano ina mtihani mkubwa wa kujibu kwa wananchi kutokna na changamoto mbalimbali ambazi zipo katika wizara ya kilimo na hivyo kutaka wizara hiyo kupitia upya mapendekezo ya bajeti yake.